Bondia Francis Cheka ameondoka leo kuelekea nchini India kuwania ubingwa WBO

BONDIA Francis Cheka, anatarajia kupanda ulingoni Desemba 17 kuwani ubingwa wa WBO dhidi yake na Bondia, Singh, katika pambano linalotarajia kupigwa nchini India katika Uwanja wa THYAGARAJ STADIUM -NEW DELIH nchini INDIA.
Mpinzani wa Cheka ni Bingwa wa Olympic aliyeibuka na Medali ya Shaba, ambapo pambano hilo linatarajia kurushwa Live na Kituo cha Tv cha SKY cha nchini Uingereza kwa kushirikiana na Televisheni ya Taifa ya India.

Mtandaohuu unawaomba wadau wa mchezo huo wa ngumi na Watanzania wote kwa ujumla kumuombea dua Bondia Francis Cheka ili aweze kuipeperusha Vyema Bendera ya Tanzania, kabla ya kurejea nchini kumkabili Bondia anayechipukia kwa kasi kurithi nafasi za wakongwe,Dullah Mbabe Desemba 25.

Chapisha Maoni

0 Maoni