Hanscana asimulia jinsi ajali ilivyotokea


Perfect255 imemkamata mmoja wa walionusurika na ajali iliyotokea jana mida flani hivi ya mchana iliyowahusisha rapper DarassaMr VS, producer Abbah pamoja na Hanscana.

Ni Hanscana ambaye alikumbwa na kipaza cha Perfect255 na kuweza kutusanua mchongo mzima jinsi ajali hiyo ilivyotokea na kudai kuwa walishindwa kuelewa chanzo cha ajali hiyo ni nn.
“Kusema kweli chanzo cha ajali tunashindwa kukielewa, sisi wote wanne tumeshindwa kuelewa kwasababu Darassa ndio ambaye alikuwa anaendesha, njiani bila sababu yoyote gari ikaanza kubinuka chini juu kisha ikaanza kubiringita takriban mara 4 kisha ikagonga kibao ambacho kilikuwa pembezoni kisha ikasimama kuelekea kule ambako tumetoka, bahati nziru kwakuwa wote tulikuwa tumevaa mikanda wote tukatoka tukiwa salama.” Aliongea Hanscana.
Kiutamu zaidi unaweza kuisikiliza story hiyo full ikisimuliwa na Hanscana baada ya k uplay hii video hapa chini.

Chapisha Maoni

0 Maoni