CLUB RAHA LEO FINAL: RAJABU SAIDI AIBUKA KIDEDEA, NDANI YA SIKU TANO ATAKIWA KWENDA INDIA

Mashindano ya Club Raha Leo yamekamilika leo, ambapo mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji tbc amekabidhi hundi kwa washindi saba na mshindi mmoja wa jumla ambaye amejinyakulia million 35 za kitanzania pamoja na safari ya kwenda nchini India kufanya show na kusoma.
Wafuatao ni washindi katika categories saba ambao wamekabidhiwa hundi ya shilingi millioni 5 kila mmoja.


AFRO POP
Charles Zuberi

TAARABU
Ramadhani Tamanda

BONGO FLAVOR
Amir Hamidu

DANCE
Rajabu Saidi

POP
Dalle Makelele

SALSA
Anafi Ramadhani

RUMBA
Musa Mohammed

Rajabu Said, ambaye pia ni mshindi katika category ya DANCE, ameibuka kuwa mshindi wa jumla ambaye amepatikana kwa vigezo vya performance kila wiki pamoja na kura za mashabiki. Mshindi wa jumla atapata fursa ya kwenda India kusoma chini ya udhamini wa Global Education pamoja na kufanya show mbalimbali. Sanjari na hilo, washindi wote wametunukiwa vyeti kutoka chuo kikuu huria Tanzania.

Akiimba wimbo kama alivyoombwa na mkugenzi mkuu, Rajabu Said ametumbuiza wimbo wa Christian Bella=Nani kama mama ambao ameubadilisha kiitikio kama dedication kwa mama yake mzazi.

Chapisha Maoni

0 Maoni