Mechi kati ya African Lyon na JKT Ruvu kusogezwa mbele

AFRICAN LYON.

MCHEZO kati ya JKT Ruvu na African Lyon uliokuwa ufanyike leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam umesogezwa mbele hadi kesho.

Msemaji wa JKT Ruvu, Ofisa Mteule Daraja la Pili, Constantine Masanja alisema jana kwamba mchezo huo umesogezwa mbele kwa siku moja na sasa utafanyika kesho Januari Mosi.

Masanja alisema kuwa kwa sasa JKT Ruvu inaendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo huo chini ya kocha wake, Bakari Shime.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu kesho ni kati ya wenyeji Toto Africans na Stand United ya Shinyanga na Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Mechi mbili zitachezwa leo; Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga wenyeji Mwadui wataikaribisha Kagera Sugar ya Bukoba, wakati Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wenyeji Mbeya City watawakaribisha Mbao FC.

Chapisha Maoni

0 Maoni