Mtazamo baada ya JPM kumtengua Lawrence Mafuru, msajili wa hazina


Miongoni mwa sifa kuu za ziada na za pekee za rais wetu Mhe. Dr John Pombe Joseph Magufuli, ni sifa ya kuwa mkweli daima toka ndani ya nafsi yake. Linapokuja suala la kuusema ukweli, Magufuli yuko very bold, atausema ukweli no matter what.


Taifa hili limefika hapa tulipofika kwa viongozi kuogopa kusema ukweli na badala yake kuuremba remba au hata ikibidi kusema uongo ili tuu kuwafurahisha watu lakini Magufuli kwenye hii falsafa yake ya hapa Kazi tuu, ni mwendo wa mchaka mchaka katika ukweli na uwazi.

Hivyo wanapojitokeza watu wakweli na wawazi kama alivyo rais Magufuli ambao ni watu ma bold wenye guts za kusema ukweli no matter what, watu hawa ni mashujaa wa taifa hili, miongoni mwa mashujaa hawa, ni aliyekuwa Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru, ambaye kutokana na kuwa mkweli too much, amepumzishwa na kusubiri kupangiwa kazi nyingine muhimu zaidi kuliko Msajili wa Hazina.

Ukweli aliousema Mafuru, ni kuwasaidia Watanzania kumwelewa vizuri zaidi rais wao, alipotoa amri ya fedha za umma kutunzwa BOT pekee, watu hawakunwelewa rais, wakadhani rais amepiga marufuku taasisi za umma kutumia mabenki binafsi, kumbe rais alimaanisha ni fedha tuu za makusanyo ndizo zinatunzwa BOT, lakini fedha za matumizi zonaendelea kuwekwa mabenki binafsi na hakuna ubaya wowote kuzifungulia Fixed Deposits.

Kuondolewa kwa Mafuru, kunatafsiriwa na wengi kuwa ni kutumbuliwa, kumbe wengi hawajui, kule sio kutumbuliwa bali ni kuandaliwa kwa majukumu mengine makubwa zaidi.

Haiwezekani mtu ufanye kitendo cha ushujaa kama kuwasaidia wananchi kumwelewa vizuri rais wao badala ya kupongezwa badala yake ukatumbuliwa, nasisitiza Mafuru ni shujaa na anastahili kupangiwa majukumu mengine muhimu zaidi. Swali ni Jee Mafuru atapangiwa jukumu gani muhimu?.

Shujaa mwingine kwenye hili la mambo ya fedha na uchumi ni Gavana wa Benki Kuu, Prof Beno Ndulu ambaye na yeye alilifafanua.

Nampongeza Lawrence Mafuru na kumtakia maandalizi mema ya kusubiri kupangiwa kazi nyingine.

Chapisha Maoni

0 Maoni