Onyo kwa atakayepoteza mtoto siku ya mwaka mpya, atakamatwa

Thobias Sedoyeka
 Wazazi na walezi mkoani Mtwara wametakiwa kuwachunga watoto wao katika sherehe za sikukuu ya mwaka Mpya, na kwamba atakaepotelewa na mtoto kwa uzembe atachukuliwa hatua za kisheria.



Wito huo umetolewa mkoani humo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Thobias Sedoyeka na kuongeza kuwa jeshi hilo halitokuwa na huruma kwa mzazi yeyote atakayetelekeza mtoto wake.

Jeshi hilo limeendelea kutoa tahadhari za kiusalama kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanakuwa waangalifu na kuepuka kuendesha vyombo vyao wakiwa wamelewa, pamoja na kuwataka wafanyabiashara wa bar kuhakikisha wanafunga biashara zao katika muda uliopangwa.

Source: EATV


Chapisha Maoni

0 Maoni