PICHA: Hivi ndivyo ilivyokuwa baada ya Messi kukutana na mtoto aliyekuwa amevaa nguo na mfuko wa plastic uliokuwa na jina la Messi




Murtaza akiwa amevalia jezi yake ya karatasi, iliyovuma sana mtandaoni
Mtoto wa kiume mwenye uraia wa taifa la Afghanistan ambaye alikuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kwa ku vaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye amefanikiwa kukutana na shujaa wake huyo kutoka Argentina.
Murtaza Ahmadi akiwa kwenye picha ya Pamoja na kikosi cha timu ya Barcelona
Picha ya Murtaza Ahmadi, mwenye miaka sita, akiwa amevalia karatasi hiyo iliyoandika nambari ya jezi ya Messi pamoja na jina lake ilivuma sana mwezi Januari mtandaoni. Mwishowe, alipokea jezi halisi kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona, ambayo pia ilikuwa imetiwa saini na mchezjai huyo.
Murtaza akiwa na jezi aliyotumiwa na Messi\
Lionel Messi alifanikiwa kukutana na Murtaza Ahmadi mjini Doha, kwa mujibu wa kamati andalizi ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.
Barcelona wamo nchini Qatar kucheza mechi ya kirafiki na Al Ahli Jumanne.
Ahmadi amefanikiwa kutembea kwenye mji huo pamoja na  kuingia uwanjani akiandamana na Messi.
Messi na Murtaza Ahmadi mjini Doha
“Ni picha ambayo ulimwengu ulitaka kuona,” aliandika mkuu wa kamati hiyo Jumanne.
“Mvulana wa miaka sita akikutana na shujaa wake, #Messi, ndoto yake ikitimia.”
Ahmadi, ambaye anatoka wilaya ya Jaghori, katika mkoa wa Ghazni mashariki mwa Afghanistan, alilazimika kukimbilia nchi jirani ya Pakistan mwezi Mei.
Murtaza ambaye picha yake ilisambazwa mtandaoni na mjomba wake ambaye ni Azim Ahmadi, raia wa Afghanistan anayeishi Australia, na baadae aliwaunganisha waandishi wa BBC Trending na nduguye, Arif – babake ambaye ni shabiki mkubwa wa Messi.

Chapisha Maoni

0 Maoni