Tanzania kuuza gesi kwenye soko la dunia

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta Ewura Felix Ngamlagosi.

Tanzania ina gesi asilia ya kujitosheleza na ya ziada na hivyo inaangalia namna ya kuiuza gesi hiyo katika soko la dunia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta Ewura Felix Ngamlagosi jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa sekta ya gesi uliondaliwa na mamlaka hiyo.

Ngamlagosi amesema mazungumzo yanaendelea kwa sasa kati ya serikali na wadau mbalimbali kutafuta namna bora na wapi pa kuwekeza katika viwanda vya kusindika gesi na kuipeleka katika masoko ya dunia.

Chapisha Maoni

0 Maoni