Video:Nyerere alipokutana na Keneth Kaunda gerezani na kushinikiza atoke



Hii video imechukuliwa wakati Mwl Nyerere alipoenda Zambia na kukutana na rais wa wakati huo CHILUBA, ambaye alikuwa kamfunga Kaunda, Mwalimu Nyerere akaomba dakika 40 za mazungumzo na rais Chiluba, baada ya hapo akaomba kwenda kumuona rafiki yake Kaunda katika gereza alilofungwa.

Akafika akaonana naye, akakuta Kaunda yuko kwenye mgomo wa kula, muda wa kumuona ukaisha akaambiwa atoke akasema hebu tufunge sote hapa mi na bwana Kaunda, kama naondoka basi naye muachieni atoke, kama hatoki nitabaki naye hapa, ikabidi uongozi wa gereza uwasiliane na Rais Chiluba akasema anaomba mazungumzo na Mwl Nyererewakayazungumza Kaunda akaachiwa.
KENETH KAUNDA KWA KAULI YAKE ALISEMA KILA LINAPOTAJWA JINA LA NYERERE NALIA NATOA MACHOZI SANA NA NINALIA.

Chapisha Maoni

0 Maoni