Barua ya Rais wa FIFA Gianni Infantino kwa Yanga

Leo May 26 2017 imetoka taarifa kutoka kwa Rais wa Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Gianni Infantino kupitia kwa Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi kuwa Infantino anaipongeza Yanga kutwaa Ubingwa wao wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania bara 2016/17.

Rais wa FIFA Gianni Infantino
Barua ya Infantino ambayo imepitia kwa shirikisho la soka TanzaniTFF inaeleza kuwapongeza Yanga, wachezaji wake, benchi la ufundi na uongozi kwa ujumla kwa mafanikio hayo waliyoyapata ya kutwaa taji la VPL kwa mara ya tatu mfululizo.

Chapisha Maoni

0 Maoni