Sakata la Makinikia:Kuna Aibu Inatunyemelea

Acacia
Hawa jamaa kweli watakuwa wametuibia lakini findings za kamati hizi kuhusu viwango vya madini na hasara tuliyopata, mimi binafsi zinanipa mashaka sana na ninaona tunaweza kuja kuumbuka hapo baadae.


Ni hivi,kama mchanga tu unaweza kuwa na madini ya thamani ya trilioni mpaka 380.9 kwa kiwango cha juu kwa miaka hiyo 19,ni wazi nchi zenye rasilimali madini duniani na zenye mikataba mizuri zingekuwa ni nchi tajiri sana katika huu ulimwngu.

Cha kujiuliza, kama hiyo ni thamani ya makinikia tu,madini yenyewe(matofali ya dhahabu) yatakuwa na thamani kiasi gani kwa miaka yote hiyo?

Alafu kingine cha kujiuliza ni kwanini findings za kamati hizi mbili za sasa na ile ya Jaji Bomani zitofautiane katika data za viwango vya madini tu lakini zifanane katika matokeo mengine ikiwemo na mapendekezo?Tukumbuke hata hadidu za rejea zimeonekana kufanana kwa maelezo ya Lissu aliyoyatoa Bungeni jana huku akiwa na ripoti ya Jaji Bomani mkononi.

Kubiwa ni kweli tumeibiwa ila hivyo viwango vya madini vilivyotajwa katika hizo ripoti,tujiulize mara mbili mbili kama vina uhalisia na hali ya nchi zingine zenye migodi tena kutuzidi.

By Salary Slip/JF

Chapisha Maoni

0 Maoni