Picha: Waziri Ummy, RC Shigella waongoza mapokezi ya Coastal Union mkoani Tanga

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwasalimia wakazi wa Mji wa Pongwe mara baada ya kuwasilia na timu ya Coastal Union ikitokea mkoani Morogoro ambapo iliweza kupanda daraja baada ya kuifunga Mawenzi ya Morogoro mabao 2-0 kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kulia akizungumza wakati alipoipokea timu ya Coastal Union mara baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao mapokezi hayo yalifanyika kwenye eneo la Pongwe Jijini Tanga kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

  Wapenzi wa soka mkoani Tanga pamoja na wananchi wakiwa wamezingira barabara ya Tanga kwenye mikoani eneo la Pongwe wakiilaki timu ya Coastal Union leo.

Mfungaji wa moja ya mabao yaliyoipandisha timu ya Coastal Union Athumani Iddi Chuji akizungumza kwenye mapokezi hayo leo.

Chapisha Maoni

0 Maoni