Sanchez afungua ukurasa wake wa mabao, Man United ikishinda 2-0

Alexis Sanchez alifunga bao lake la kwanza akiichezea Manchester United baada ya timu hiyo kuishinda Huddersfield na hivyobasi kuisukuma katika eneo la kushushwa daraja.


Baada ya kipindi cha kwanza Romelu Lukaku aliipatia United uongozi kunako dakika 55 baada ya kupokea krosi nzuri.

Sanchez baadaye alichezewa rafu na beki wa Huddersfield Michael Hefele na hivyobasi kutunukiwa mkwaju wa penalti aliopiga ukapunguliwa na kipa kabla ya kuupata na kufunga.

Chapisha Maoni

0 Maoni