Katika
makala iliyopita juu ya siasa za Tanzania na hatima ya maendeleo ya taifa,
nilizungumza kuhusu sera mbalimbali na madhara ya siasa kwenye utekelezaji wa
sera, ambapo nilianza na sera ya elimu ya mwaka 2014. Nilizungumza kipengele
kidogo kabisa cha elimu ya awali ambacho kimeainishwa katika sera ya elimu na
mafunzo ya ufundi. Nilizungumzia mazingira gani ambayo mtoto anatakiwa
kutengenezewa ili kumwezesha kushika kile anachofundishwa kulingana na umri
wake. Ikumbukwe pia, kwenye sera, umri uliowekwa kuwa ni umri wa mtoto kupata
elimu ya awali ambayo ni ya lazima ni miaka 3-5, na ni umri ambao kisaikolojia
ni umri wa makuzi ya awali ya mtoto yaani, Early childhood stage, hatua
ambayo leo nitaizungumzia kinagaubaga pamoja na umuhimu wake katika uzalishaji
rasilimali watu, moja ya kiolezo muhimu kabisa katika
mazingira ya mtoto aliye
katika hatua ya elimu ya awali.
Makuzi
ya awali ya mtoto yanaanzia miaka 2-5, umri ambao ndani yake ni umri wa elimu
ya awali iliyoainishwa kwenye tamko la sera ya mwaka 2014. Sifa kubwa ya umri
huu ni kwamba, mtoto hukua zaidi misuli
mikubwa, kuliko midogo, misuli ambayo humfanya kila kazi anayoifanya, aifanye
kwa nguvu nyingi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, mtoto mwenye umri wa
miaka 2-5 huwa ana uwezo mkubwa sana wa kutumia misuli mikubwa katika kufanya
kazi, misuli kama ya mikono, miguu na ya mabega. Katika kipindi hiki, mwendo wa
ukuaji wa misuli midogo kama ya viganjani huwa ni ndogo sana, na kutokana na
udogo wa mwendo wa kukua kwa misuli hii, mtoto aliye katika umri huu huwa na
uwezo mdogo sana wa kufanya kazi ndogo kama kudhibiti mwandiko kwenye daftari. Hapa ndipo wataalamu wa
saikolojia hushauri mtaala wa elimu uwe wenye mlengo wa kazi tu (activity
oriented curriculum) ambapo hii humsaidia mtoto kuendeleza makuzi ya kawaida ya
mwili ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa misuli yote. Mmoja kati ya
wanasaikolojia wanaoshauri hili ni Maria Montensori katika kitabi chake cha
Absorbent Mind.
Hali
kwenye shule zetu ikoje?
Katika
umri kama huu, kwanza kuanzia mavazi ya mtoto huwa ni tofauti kabisa na mavazi
ya watoto wengine kama watoto walio katika madaraja ya mbele. Mfano, kaptura ya
mtoto wa umri huu kitaalamu inatakiwa kuwa na lastic kiunoni, na si belt.
Je, wajua ni kwa nini? Hii ni kutokana na ukweli kwamba, mtoto wa umri huu,
kama nilivyosema awali, huwa na uwezo wa misuli mikubwa kuliko misuli midogo,
yaani more large muscles than fine
muscles. Maana yake nini? Mfano, ni rahisi zaidi kwa mtoto wa umri huu
kuvuta kaptura yake na kukojoa, kuliko kufungua zip na belt, kwa maana,
kufungua belt na zip huhitaji misuli midogo, wakati kuvuta kaptura hutumia
misuli mikubwa.
Maana
yake nini kwa watoto walioko kwenye shule ya awali?
Nimefanya
uchunguzi yakinifu na kugundua kwamba, watoto katika shule nyingi za awali
wanafundishwa kuandika tarakimu na hata baadhi ya herufi, kitu ambacho ni sawa
na kuandika 0 kwenye maji. Kwa nini? Kitendo cha kuandika huhitaji misuli
midogo ya mtoto, misuli ambayo katika umri huu huwa haiku vizuri, hivyo ni
vigumu kwa mtoto ku-control kiganja
chake na kuandika herufi au tarakimu kwenye daftari ambalo walimu wanawahitaji
watoto kuandika. Kama haitoshi, kuna shule zingine ambazo zinasisitiza mtoto
awe na daftari la mistari mikubwa na midogo, ili kwenye hiyo mistari midogo
ndimo mtoto anatakiwa kuunda herufi yake, nasema hili kamwe ni vigumu
kufanikiwa. Msisitizo: katika umri tajwa
wa mtoto kuanza elimu ya awali kwa lengo la kumtengenezea msingi wa madaraja
mengine, mtaala haujaangalia vizuri saikolojia ya mtoto na hivyo, si rahisi
kutengeneza msingi wa kuandika kwa mtoto mwenye umri uliotajwa kwenye sera.
USHAURI.
ü
Mtaaala
wa elimu ya awali unatakiwa uwe na mlengo wa kuendeleza makuzi ya awali ya
mtoto na si kuandika, maana si umri sahihi wa mtoto kujua kuandika kwa umri
wake, na;
ü
Mtaala
ujumuishe zaidi kazi za mwili (physical activities) ili kuijenga saikolojia ya
mtoto katika umri huu.
Usikose
kufuatilia makala zangu ambazo zinachambua sera
ya elimu na mafunzo ya ufundi na mitaala yake kwa ujumla.
Wasiliana
na mimi kwa nambari 0759 947 397 au nitumie ujumbe kwa barua pepe anwani jumahussein59@yahoo.com
Soma
makala kwenye blog yangu ili tufahamishane mengi.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA