Dar Es Salaam
Leo kuna baadhi ya vijana waliositishiwa ajira zao walikuwa ofisi ya
utumishi na utawala bora dar es salaam vijana hao ni moja ya kundi kubwa
la watu 3000 walioajiriwa mwezi june 2016 na kusitishiwa ajira zao
baada ya kusainishwa mikataba na kuanza kazi vijana hao leo wamefanikiwa
kuonana na waziri wa utumishi wa umma Angellah Kairuki pamoja na katibu
mkuu utumishi wa umma vijana walikuwa na swali moja la kuuliza kwa
waziri na katibu mkuu wizara waliwauliza ni lini watarudishwa kazini ?
waziri kairuki alijibu kuwa yeye hajui kuwa
ni lini watarudishwa kazini
maana hata yeye anapokea maelekezo kutoka juu na kutekeleza kairuki
alijibu kuwa hata yeye ofisini kwake hili zoezi analiona kero anatamani
hata liishe leo ila hana jinsi kwa sababu halipo chini ya ofisi yake kwa
sasa katibu mkuu aliongezea na kusema kama zoezi lingekuwa kwao
walikuwa wanatamani likamilike hata leo hii viongozi hao walisema
mwenye mamlaka ya zoezi hilo ni la mhe.rais hivyo na wao hawajui juu ya
swala la uhakiki litaishi lini.
waziri kairuki na katibu waliomba vijana hao waliositishiwa ajira
kujishughulisha na shughuli zingine kuliko kusubiri maana zoezi hilo
haliratibiwi na ofisi hivyo pia vijana hao waliuliza swali la nyongeza
je ajira zao zipo au zimefutwa ? waziri kairuki alisema kuwa kuna mawili
wayategemee kutoka kwa mh.rais kufutwa ajira na kuanza upya au
kutofutwa alisema hayo yote wayategemee kwa sababu serikali imebadilisha
muundo wake hivyo taratibu za ajira mpya zaweza badilika kwa sababu
serikali hii itakuwa imefanya mabadiliko.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA