Kuna taarifa kuwa Waziri wa Maliasili na
Utalii, ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mkuu wa Pori la Burigi
mkoani Kagera, kwa kosa la mkuu huyo kukamata ng’ombe 400 walioingizwa
na raia wa Tanzania na Rwanda porini humo.
Pamoja na mifugo, wenye ng’ombe hao wamekamatwa wakiwa na nyara (wanyamapori waliouawa).
Kusimamishwa kwake kumetokana na shinikizo la Wabunge wa Kamati ya
Utalii, Maliasili na Mazingira wakiongozwa na Mbunge Musukuma, waliotaka
mifugo hiyo iachiwe mara moja bila masharti.
Inaelezwa kuwa Mkuu wa Pori anayeitwa Bigilamungu, alihoji uhalali wa
kuachiwa kwa ng’ombe pamoja na watuhumiwa hao waliokamatwa wakiwa na
nyara za Serikali. Kitendo cha kusita kutekeleza amri hiyo, kumegharimu
kazi yake!
Sasa wabunge wanashinikiza hata Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa naye asimamishwe kazi!
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA