Benki ya serikali Twiga Bancorp yaishiwa mtaji.

OT yaingilia kati na kuvunja menejimenti pamoja na bodi ya benki.


Benki ya serikali Twiga Bancorp imechukuliwa na BOT kutokana na kuishiwa mtaji.

Benki Kuu imechukua udhibiti wa Benki hiyo baada ya mmiliki (serikali) kushindwa kukuza mtaji huku ikiwa na mzigo mkubwa wa madeni.

Aidha BOT imeivunja Bodi na Menejimenti ya Benki hiyo.

Katika Mkutano wake na wanahabari leo Oktoba 28 jioni katika makao makuu ya BOT Dar, Gavana wa BOT Prof. Benno Ndulu amesema Twiga imekatika mtaji na ina madeni lukuki yasiyolipika, hivyo haiwezi tena kutoa huduma hadi hapo mwekezaji atakapopatikana.

Ndulu amesema wamechukua hatua hiyo kuwalinda wateja na kulinda maendeleo ya sekta ya kibenki nchini

Chapisha Maoni

0 Maoni