Chuo kikuu cha Dodoma kimeendelea kutafuta suluhu ya ombi la UDOSO ili kukamilisha mchakato wa kukata moja kwa moja pesa anayodaiwa mwanafunzi kutoka kwenye pesa yake ya kujikimu.
Ombi hili liliwasilishwa na serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dodoma (UDOSO) ambapo ilikaa na menejiment ya chuo ili kulifanyia kazi ombi hilo. Mahenga Blog ilimtafuta rais wa shirikisho chuo kikuu cha Dodoma Bw. Bruno Julian Kayoza kulitolea ufafanuzi suala hili, na akizungumza kwa niaba ya UDOSO, alikiri kuwa mpango huo ni kweli upo na chuo bado kinaufanyia kazi ili kufikia muafaka wa ombi hilo.
Mpango huu unatarajiwa kuwasaidia wanafunzi wanaotegemea pesa hiyo ya kujikimu kulipa ada yao huku wakiendelea na masomo na kufanya udahili bila bughudha.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA