Maisha ya shost na mume wake hayakuwa mazuri kihivyo, wote walikuwa
wajiiriwa wa serikali na walibahatika kupata watoto wawili, wakiume
miaka mitano na wakike miaka mitatu. Kila wakikaa na mume wake
walijaribu kujipanga jinsi ya kusomesha watoto, na kuwa hata na kibanda
chao wenyewe badala ya kupanga nyumba.
Bi shost alifukuzia nafasi za masters kila zikitoka kazini, na alianza
na maombi milango ifunguke. Wakisema kila kitu kina wakati wake si
utani, siku shost alipopata waraka wa kumfahamisha anatakiwa kujiunga na
chuo kikuu kilichopo Botswana kwa masomo yake ya shahada ya uzamili.
Walikaa chini na mume wake, wakapanga kuwa, akifanikiwa kumaliza masomo
atafute kazi kule ili watoto wapate elimu bora pia waweze kuweka pesa ya
kujenga nyumba nyumbani. Bishost alifanya tafrija kidogo ya kuwaaga
ndugu na jamaa wa karibu na kuondoka.
Alikuwa na utaratibu wa kuongea na mume wake kila siku jioni na watoto
weekend kwakuwa mara nyingi anapopata nafasi ya kupiga simu watoto
wanakuwa wamelala. Miezi kama minne baada ya kuondoka tabia ya mume
ikaanza kubadilika, anapopiga simu inakuwa imezimwa, akumuuliza ni
visingizio vingi tu. Yule dada alitafakari hili akaamaua kumwambia mume
wake, kama wewe uko busy, basi wanunulie watoto simu ili nikipiga
niongee nao maana kama mama huwa sina amani nikiwa mbali nao.
Simu ilinunuliwa na baba akijua amepata nafuu ya kusumbuliwa. Sasa baba
hakwenda mbali sana, Alianza kutoka na rafiki wa karibu sana wa
bishost, anaeitwa Clara, aliyempa mkanda wote huo bishost ni mtoto wa
kiume wa miaka mitano, kwa kifupi, Clara alianza kuplay mother figure
kwa watoto, alimpeleka yule boy kwa dentist, weekend anawapeleka wakale
ice cream, kwenye mabembea. Basi mtoto alianza kutiririka, mama akawa
oh, mpe aunt Clara asante nyingi, akijua ni shost anamsaidia, zali
lilikuja mtoto alipoendelea nitamwambia kesho akiamka, khe wewe kwani
unalala kwake, hata si analala chumbani kwako.
Bi shost hakuongea na mtu, alinunua ticket na kuja na kumkuta kweli aunt
Clara ameenea sitingroom akiangalia TV na mr akiwa na khanga moja.
Ndoa ilisalimika na baba alikusanya watoto wote walielekea Botswana.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA