Waziri wa vijana sera na mipango ,walemavu Jenista Mhagama jana alikuwa
mkoani Simiyu kwa ajili ya kufungua tamasha la vijana linalohusu fursa
mbalimbali zinazopatikana nchini zinatumiwaje na vijana.
Waziri wa vijana alitoa ahadi kuwa atawapa ardhi vijana ili wajikite
kwenye kilimo pamoja na hivyo vijana waliwasilisha kero zao
zinazohusiana na ajira kusitishwa na wengine walioajiriwa mwezi May 2016
waliosimamishwa kazi na serikali huku ikiwa imewasainisha mikataba ya
kazi na kuanza kufanya kazi lakini walisimamishwa bila kulipwa stahiki
zao na bila kuambiwa watarudishwa lini kazini.
Vijana mkoani Simiyu na mikoa jirani walimuomba Waziri huyo jana kuokoa
wimbi la hawa vijana ambao hawajui hatima yao na familia zao.
Waziri Mhangama alidai kuwa ajira ktk taifa letu ni tatizo lakini
alikili kujitaidi jinsi ya uwezo wake kutatua kero zinazowakabiri vijana
nchi maana vijana ni nguvu kazi ya taifa alisema.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA