Serikali ya Tanzania imesema kwamba kulingana na takwimu inaonesha kuwa
ukosefu wa ajira kwa vijana nchini Tanzania umepungua kwa asilimia
mbili, kutoka asilimia 13.7 mwaka 2012 mpaka asilimia 11.7 mwaka huu.
Akizungumza leo bungeni, mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na
majibu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na
Walemavu Mhe. Anthony Mavunde, amesema licha ya kupungua huko kwa
ukosefu wa ajira, serikali imeweka mipango ya kuwawezesha vijana kuwa na
wigo mpana wa ajira nchini.
Mhe. Mavunde amesema kuwa kwa takwimu hizo Tanzania ni nchi inayoongoza
kwa kutoa ajira kwa vijana wengi zaidi kushinda baadhi ya nchi za Afrika
Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA