Dar es Salaam
Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Serikali kupambana na tatizo sugu la
ujangili, kimenasa bunduki 11 ambazo zinasadikiwa kutumika kufanya
ujangili na kukamata watu wanne zaidi.
Taarifa zilizopatikana jana zimelidokezea gazeti hili kuwa bunduki hizo
zilikamatwa nyumbani kwa mbunge wa CCM (jina tunalihifadhi) ambaye bado
anasakwa na kikosi kazi hicho.
Matukio hayo yamekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kutaja
jina la mtu anayeitwa Mpemba kuhusika na ujangili kwa muda mrefu wakati
alipotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii na kushuhudia pembe
50 za ndovu zilizokamatwa na watumishi wa wizara hiyo.
Siku hiyo, Rais aliwaambia watu aliowaita “vijana” waendelee na kazi yao
ya kukamata wauaji wa tembo, akiwahakikishia kuwa Serikali ipo na
kuwataka wasiogope mtu yeyote yule.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA