Akiongea kwa masikitiko huku akitoa machozi, amesema amesikitishwa sana
na Chama cha Mapinduzi kwan kwa muda mrefu amekua akikipigania Chama cha
Mapinduzi kwa Hali na Mali Lakini leo kinamtoa machozi.
Akiandika kupitia Gazeti lake la Ijumaa Wikienda lakini Pia kupitia
ukurasa wake rasmi wa Facebook amekilalamikia chama cha mapinduzi
kuendelea kumzungusha kuhusu malipo yake zaidi ya mwaka mmoja na nusu
sasa tangu Afanye Biashara na Chama hicho, aliendelea kulalamika kua
Amefanya jitihada za ziada kumpigia Katibu mkuu wa Chama hicho Abdalah
Kinana bila mafanikio kwani amekua hapokei simu zake wala kujibu sms.
Anasema Pamoja na kwenda ofisi za Chama hicho Lumumba alikutana na mweka
hazina wa Chama hicho Mamma Zhakia Meghji lakini aliambulia kupewa Maji
ya Kunywa Bila kupata Pesa zake.
Kinacho muuma Bw Shigongo ni alivyoacha Biashara zake na Kufanya Kampeni
karibu Mikoa 10 huku akimpigia Kampeni Rais mstaafu wa wakati huo Dr.
Jakaya Kikwete.
Akiongea kwa masikitiko amesema mpaka sasa Mali zake zipo Mbioni kupigwa
Mnada wakati wowote kutokana na kwamba ndizo alizoweka Bond ili aweze
kupata mkopo ambao alitumia ku supply baadhi ya materials kipindi cha
Kampeni za Uchaguzi 2015.
Kwa maelezo zaidi ameahidi kutoa week ijayo katika ukurasa wake na
kwenye Gazeti la Wikienda. Na Amesema ataweka wazi ni Kiasi Gani
anakidai chama cha Mapinduzi.
Pole sana Brother Eric Shigongo, Endelea kupigania Haki yako ili
wakulipe, ni Matumaini yangu Mwenyeketi wa Chama cha apinduzi amesoma
Ujumbe wako na atalifanyia kazi ili uweze kulipwa Pesa zako
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA