Serikali ya mkoa wa Singida imetatua mgogoro wa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Singida.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mapema leo katika mji mdogo wa
Ilongero mkuu wa mkoa wa Singida Eng. Mathew Mtigumwe amesema kwamba
makao makuu ya wilaya yatajengwa katika kijiji cha Ilongero kata ya
Ilongero kama ilivyopitishwa na vikao halali vya wilaya na mkoa.
Mgogoro huu ulitokana na uamuzi wa Baraza La madiwani Halmashauri ya
wilaya ya Singida wa tarehe 28 /10 /2016 kupitisha azimio la kujenga
makao makuu ya wilaya katika kijiji cha Kinyamwambo kata ya Merya
katika Mazingira ya ghiliba, rushwa, hujuma na mizengwe kukidhi matakwa
ya viongozi wachache
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Singida ameeleza kwamba watu wachache wenye
masilahi binafsi hawawezi kubadilisha maamuzi ya wananchi walio wengi na
ametoa Agizo kwa viongozi wa Halmashauri waanze kuhamia Ilongero
kuanzia Sasa na ametoa muda wa miezi 6 mchakato wa kuhamia Ilongero uwe
umekamilika.
Ushindi huu unatokana na Kamati Maalum iliyoundwa kwa niaba ya wananchi
wa Singida kaskazini kuandaa pingamizi lenye hoja za msingi kupinga
uamuzi wa Baraza La madiwani kupeleka makao makuu ya wilaya katika
kijiji cha Kinyamwambo kata ya Merya ambapo Kamati Maalum iliwasilisha
pingamizi kwa mkuu wa mkoa Mnamo tarehe 21/11 /2016.
wanaohujumu wananchi wa Singida kaskazini kwa masilahi yao binafsi wanafahamika kwa majina na kwa mbinu zao.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA