Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL
kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa
vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.
Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi hicho
hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy amewahi
kuzifanya ili kuomba wayamalize.
Hitmaker huyo wa Wanjera amesema katika urafiki wao wote na Diamond, ni
yeye ndiye alikuwa mwaminifu (loyal) zaidi katika kuuenzi lakini kuna
wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa
vinavyohusiana na kazi.
Amesema mara zote alikuwa akimshirikisha kwenye mipango yake ikiwa ni
pamoja na kumsikilizisha nyimbo zake kabla ya kutoka ili kumuomba
ushauri na kutolea mfano alivyomsikilizisha wimbo wake Tupogo na
kumweleza kuwa amepanga kuongeza vionjo vya saxaphone kwa kumtumia King
Malou. Hata hivyo anadai kuwa siku chache baadaye alishangaa kumkuta
Diamond akiwa na mpiga saxaphone huyo akiingia kionjo kwenye wimbo wake
‘Number 1’ katika studio za MJ Records.
“Nikajiuliza kuwa pengine labda alikuwa na wazo kama hilo, sikutaka
kujiuliza mengi, unajua sometimes ukijiuliza mengi utaenda far zaidi,
nikauchuna tu,” alisema Ommy.
Anasema baadaye alisikia akimuambia Marco Chali kuwa amchomee CD kwakuwa
anasafiri na walipomaliza Ommy alimuuliza kuhusu safari hiyo lakini
Diamond alimuambia kuwa alikuwa akimdanganya tu producer huyo wa MJ
Records na kwamba hakuna safari yoyote.
“Kesho yake naona anapost picha yupo kwenye ndege, nikajiuliza ‘huyu si
nilimuuliza jana kama anasafiri, si ni mwanangu’, nikasema anyway labda
ni safari imejitokeza ghafla you never know,” ameeleza Ommy.
Baadaye mshkaji wao Halima Kimwana alikuja kumwambia kuwa Diamond
alienda Afrika Kusini kufanya video yake kitendo kilichomwacha na
maswali mengi lakini anadai alipuuzia. Amesema baada ya muda ndipo
Diamond alipofanya uzinduzi wa video ya Number 1 na yeye mwenyewe
kualikwa.
Amesimulia tukio jingine ambalo lilimuumiza ni baada ya kumuomba Diamond
waende pamoja Marekani kwenye tuzo za Afrimma kwa gharama zake mwenyewe
ili amsaidie kumtafutia connection.
“Sasa kila siku nikiuliza safari lini naona mtu anaingilia huku anatokea huku.”
Anadai swahiba wake huyo aliendelea kumchenga hadi alipokuja kugundua
amesafiri bila kumwambia na siku hiyo akawa hapokei simu zake. “Baada ya
kupita masaa mengi, jioni anakuja kunicheck yuko transit South Africa
‘mwanangu ilitokea ghafla nikasafiri.’ Kwahiyo nikajiuliza nikasema hapa
kuna style za kupunguzwa. Kibinadamu unajua lazima uchekeche.”
Ommy pia alielezea jinsi ambavyo alikuwa mtu wa kwanza afanye collabo na
Davido na alikuwa tayari kutoa $3,000 lakini baadaye Sallam, meneja wa
Diamond, alikuja kumweleza kuwa Dangote yupo tayari kutoa $5,000 ili
wafanye naye. Anasema aliachana na collabo hiyo na kutafuta nyingine na
Iyanya ambayo nayo pia alikuja kugundua baadaye rafiki yake huyo
ameshaiwahi.
Hata hivyo Ommy amedai kuwa kitendo cha yeye kumtumia Wema Sepetu kwenye
video ya Wanjera ilikuwa kama sababu tu ya Diamond kuvunja ushkaji
wake. Amesema ni kwasababu amekuwa na urafiki na Wema hata kabla ya
kukutana na Chibu na kwamba hadi ‘first kiss’ yao aliishuhudia kwa macho
yake.
Ommy ambaye jina lake ni Omari Nyembo, amesema kukosana kwao hakukuwa
sababu ya yeye kumchukia pia Wema kwakuwa urafiki wao haukusika na
kwamba kipindi Ommy anaenda SA kufanya video hiyo, Wema alikuwa na
uhusiano na mwanaume mwingine na kukanusha kuwahi kutoka naye kimapenzi.
“Kwahiyo nikaona kuna suala lilikuwa kwamba mtu ametafuta sababu. Hebu
niambie Wema amekuwa na mahusiano na watu wangapi wengine ambao leo hii
bado unaona D yuko nao close? Kwanini nilipokuwa naye mimi tu ndio
imekuwa tatizo?” amehoji staa huyo.
Kuhusu tuhuma za kutaka ‘kupumuliwa’ zilizotolewa na Diamond kwenye post
yake ya Instagram dhidi yake, Ommy amesema pale ‘mtu anapotaka kukutana
hakuchagulii tusi.’
“Sometime unapoitoa kauli, huwezi kujua itamwathiri mtu kwa kiasi gani,
pengine itamwathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu kuna mtu ataichukua ile
kauli kiushabiki. Hata kwenye comments, mimi ninaweza kuzima comments
zangu kwenye Instagram lakini nimeziacha na ukisoma comments utaona
kabisa mwingine anakutukana ‘we shoga.’ Lakini as long as mimi ninajua
mzima hainiathiri, kwanza hakuna tusi jipya, imeanza kutukanwa mimba!”
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA