Rais
John Pombe Magufuli amemwalika Rais wa Jamhuri ya Zambia, Edgar Lungu
kufanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia Novemba 27 hadi 29, 2016.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.
Augustine Mahiga amesema katika ziara ya rais Lungu atatembelea vitengo
na sehemu muhimu zinazounganisha nchi ya Tanzania na Zambia kiuchumi.
“Rais Edgar Lungu amealikwa na Dk. Magufuli kutembelea nchini kuanzia
Jumapili ya Novemba 27 hadi 29, 2016. Katika ziara yake atatembelea
vitengo na sehemu mumihu vinavyounganisha nchi na Zambia kiuchumi ikiwa
ni pamoja reli ya Tazara,” amesema.
Ametaja sehemu nyingine atakazotembelea Rais Lungu kuwa ni Bandari ya
Dar es Salaam, na kituo cha mizigo kinachohifadhi mizigo inayokwenda
Zambia kabla ya kwenda bandarini.
“Siku ya mwisho ya ziara yake, atembelea bandari ya DSM kabla ya
kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudi nchini kwake,” amesema.
Aidha, Mahiga amesema Rais Lungu na Magafuli watasaini baadhi ya
mikataba ikiwemo ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara ) ili
kulifufua shirika hilo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA