Mchezaji nyota wa club ya Real Madrid na mzaliwa wa Ureno, Christiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 31 amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea club hiyo kwa miaka mitano mingine.
Nyota huyu ataichezea club hiyo hadi 2021 ambapo atafikisha umri wa miaka 41, na ndoto yake kuu ikiwa ni kuendelea kutikisa nyavu.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari chetu, Christiano Ronaldo ndiye mchezaji anayelipwa kiasi kikubwa cha fedha kwenye club hiyo, kiasi cha pound 365,000 kwa wiki.
Kwenye mkataba wake mpya, kiasi hicho cha pesa hakijabadilika na hivyo ataendelea kulipwa hivyo kwa miaka yote ya mkataba wake.
Aidha, Christiano Ronaldo amesema, bado ana miaka kumi ya kuonesha makeke yake kabla hajastafu kandanda.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA