Mbunge wa baraza la uwakilishi Zanzibar Mhe. Jaku Hashimu Ayoub amehoji daraja la kigamboni kuitwa jina la Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye tayari ana kumbukumbu nyingi hapa nchini kama uwanja wa kumataifa wa ndege na ukumbi wa mkutano Dar.
Mhe. Ayoub alilielekeza swali lake kwa waziri wa ujenzi Mhe. Ngonyani huku akimuomba kuweka usawa katika namna ya kuwaenzi viongozi waliotoa mchango mkubwa hapa Tanzania. "Mhe. Aboud Jumbe ana historia ya kukaa Kigamboni kwa muda mwingi, na mchango wake pia ni kuleta demokrasia ya baraza la uwakilishi Zanzibar, kwa nini daraja hilo lisipewe jina la Aboud Jumbe.." aliuliza Hashimu.
Akijibu swali hilo, waziri wa ujenzi amemtaka mbunge huyo kupeleka mapendekezo kwa madaraja mengine ambayo bado yanajengwa yanaweza kuitwa jina hilo kama anavyotaka. "Mpango wa ujenzi wa madaraja ulianza toka awamu ya tano chini ya rais wa kwanza Baba wa taifa ambapo katika mpango wa kwanza wa miaka sitini, madaraja matano yalipendekezwa kujengwa, yaani Kigamboni, Rufiji, Maragalasi, Kilombero...hivyo yatakapokamilika yanaweza kuitwa kwa jina la viongozi hao wengine..." amesema Mhe. Ngonyani.
Aidha, Mhe. Hashimu ameitaka serikali kuweka namna nzuri ya kuwaenzi viongozi waliotoa mchango mkubwa kwa taifa kwa usawa. "serikali iangalie namna nzuri ya kuwaenzi viongozi, Baba wa taifa anazo kumbukumbu nyingi na hata Zanzibar kuna barabara zinazoitwa jina lake..."
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA