MWIGULU NCHEMBA: walioko magerezani ukiwahoji mmojammoja, unaweza kusema gereza limeshirikilia malaika!

Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwigulu Nchemba amewataka wabunge kuacha kulilalamikia jeshi la polisi kuwa linawabambikiza kesi watu wengi wakiwemo wanasiasa na watoto chini ya umri wa miaka kumi na nane (18) na kuwataka wabunge kwa kuwa ni viongozi watembelee kwenye magereza hayo ili wakajaribu kufuatilia mienendo ya kesi hizo.


Akijibu swali la mbunge la Mbunge Ester Matiko aliyetaka kujua hali ya ucheleweshwaji wa kesi za mahabusu ambapo asilimia 35 ya mahabusu hao ni kesi za kubambikizwa, je nini kinababisha kesi hizo kucheleweshwa na mahabusu kuendelea kukaa gerezani.

Mhe. Mwigulu Nchemba amekanusha kuwa, si kweli asilimia 35 ya mahabusu wana kesi za kubambikizwa na amewataka wabunge wasizungumzie kwa ujumla. "..nimetembelea magereza, na kati ya mahabusu niliowahoji kama wametenda kosa, ama la, ni mmoja tu aliyekubali, lakini wengine wote walikanusha kuwa hawakutenda makosa, kwa hiyo ukiwasikiliza unaweza kusema gereza limeshikilia malaika, lakini ukifuatilia ndipo utajua kuwa wanastahili kuwepo mahali hapo.." Amesema waziri.

Akiendelea kujibu swali la nyongeza la Mhe. Gimbi, Mhe. Mwigulu amesema, ucheleweshwaji wa kesi ni kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kisayansi vya uchunguzi, na serikali inaifanyia kazi changamoto hiyo.

Aidha, Mhe. Mwigulu amewataka wananchi kuliamini jeshi la polisi kuwa, wanafanya kazi kwa kiapo, hivyo kumekuwapo na kuwachukulia hatua za nidhamu kwa polisi wanaobainika kufanya kazi pasi nakuzingatia kiapo chao.

Chapisha Maoni

0 Maoni