Jela yamuita Samuel Eto’o

Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Samuel Eto’o na timu ya taifa ya Cameroon huenda akafungwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya waendesha mashtaka kumhusisha na kashfa ya kukwepa kulipa ushuru nchini Hispania.


Eto’o kwasasa anakipiga Antalya Spor wa Uturuki, ni mmoja wa wachezaji ambao waliowahi kuchukua tuzo ya Mwanasoka Afrika mara nne.



Mahakama ya nchini Hispania imeanza kusikiliza kesi ambayo tayari imeeleza kuda kitita cha cola million 15.1 kwa mshambuliaji huyo kwa madai alikwepa kodi wakati wakati akiichezea Barcelona.
Taarifa zinasema, mwakilishi wa Eto’o, Jose Maria Mesalles Mata ndiye anaweza kukutana na adhabu hiyo kama mwanasoka huyo raia wa Cameroon hatatokea.

Chapisha Maoni

0 Maoni