Amesema taarifa hizo zitaisaidia serikali kuzitwaa ardhi hizo kwa kuwa
raia wa kigeni hawaruhusiwi kumiliki ardhi nchini na kufanya hivyo ni
kukiuka sheria.
Akitoa hotuba kwenye mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wapima Ardhi
Tanzania (IST), Mhe. William Lukuvi amesema anayeruhusiwa kumiliki ardhi
nchini ni raia wa Tanzania pekee na kuongeza kwamba kwa watanzania
waishio nje ya nchi na kuukana uraia wao nao hawataruhusiwa kumiliki
ardhi bali watapewa ardhi kama ilivyo kwa wawekezaji kutoka mataifa
mengine.
“Mtu akishaukana uraia wa Tanzania hana haki tena kama raia wa Tanzania,
hivyo atamiliki ardhi kama mwekezaji na siyo raia, ardhi itabaki kuwa
ya Watanzania tu, tutawasaka wale wote ambao wanamiliki ardhi kinyume na
sheria za nchi,” amesema Mh. Lukuvi.
Aidha, Mhe Lukuvi amewataka wapima ardhi Tanzania kuhakikisha wanatimiza
lengo la serikali la kupika na kutoa hati 400,000 ifikapo mwezi Juni
mwaka 2017 pamoja na kutenga maeneo ya wafugaji kila wapimapo ardhi.
Wadau hao wa upimaji ardhi wamesema, watahakikisha wanatimiza lengo la
serikali la kupima na kutoa hati 400,000 ifikapo Mwezi Juni2017 kwa
kutumia vifaa vya kisasa sambamba na kuwekeza hasa mikoani ili kutoa
fursa sawa kwa watanzania kupata hati za ardhi yao.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA