ARUSHA: Wakili
John Mallya (CHADEMA) leo amesema wamefungua kesi Mahakama Kuu kutaka
Mbunge Godbless Lema afikishwe Mahakamani baada ya kukaa Mahabusu kwa
muda wa siku 6 kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Wakili huyo amedai kuwa mtuhumiwa anapaswa kukaa masaa 24 tu kwa mujibu
wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai. Hivyo kesi imeadhimia kuwataka
RCO, Mwenasheria Mkuu na IGP wamlete Lema Mahakamani kwa amri ya
Mahakama.
Aidha kwa upande wa Jeshi la Polisi limeeleza kuwa upelelezi juu ya Mbunge huyo wa Arusha Mjini bado haujakamilika.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA