Usipotenda kwa umakini unaweza kujichukia na mambo mengi hayatoenda
sawa. Kila mtu anahitaji mtu mwenye nguvu zaidi yake amnyanyue. Na mtu
mwenye nguvu ni yule mwenye busara. Kwasababu hata kama mtu ana nguvu
kiasi gani kama hana busara atakuja kukamatika tu na asione njia ya
kupita. NI MUHIMU sana kukaa karibu na mtu mwenye hekima na kujifunza
kutoka kwake.
Matatizo kila siku yanapiga hodi na yanahitaji hekima kuyatatua. Ni
Muhimu sana kuwa na busara kwasababu ndio yenye kutusaidia kufanya
maamuzi yaliyo bora katika maisha yetu. Itatusaidia kujenga familia zetu
na hata taifa letu. Pesa haiwezi kufanya hivyo. Haiwezi hata kidogo.
Bali ukiwa na pesa na busara umebarikiwa kweli kweli. Jitupe chini na
mshukuru Mungu ukiwa na hivyo vitu viwili vitakupatia Great Comfort. NO
man can be Great without WISDOM. DRINK A CUP OF WISDOM.
Basi tumuombe Mungu aliyejuu atubaliki kwa busara na hekima. Ili tutende
katika usahihi na tujenge nyumba zetu na familia zetu vyema katika
upendo na umoja. Tujenge nyumba zenye heshima na watoto wenye utii kwa
wazazi wao.
Kwa njia hii pekee tunaweza kuwa na matumaini. Hakuna mwanamume mwenye
akili anaweza kufurahia kurudi kwenye nyumba ambayo haina order.
Mwanaume mwenye akili hujenga nyumba yenye nidhamu na utii. Na ufanya
maamuzi yake kwa umakini bila papara.
Ni kitu gani kinachoweza kuweka familia pamoja kama sio hekima? kama sio
busara? Sio busara ambayo hutusaidia kufanya maamuzi yaliyo bora? Na
sio maamuzi ya leo tu na hata yenye faida kwa siku za mbeleni?
Kila tendo letu tunalofanya huunda kitu. Hii iwe kwa kujitambua au
kutokujitambua. Lakini wale wanaotenda kwa kujitambua ndio wanaoendelea
zaidi kuliko wale ambao hawatendi kwa kujitambua. Kwasababu wana uwezo
wa kuchagua kilicho bora kwao na kufuata njia iliyo sahihi. Kuna matokeo
katika kila matendo yetu. Tutavuna tunachopanda.
Kushindwa kufanya chaguzi bora ambazo zitakufanya usonge mbele ni
udhaifu wa kiakili. Ndio maana kuna usemi unaosema kabla haujatenda kitu
chochote fikiri kwakuwa huwezi kurudisha muda nyuma ukiisha tenda jambo
na majuto ni mjukuu. Kwahiyo binadamu anatakiwa kuwa makini katika
fikra na matendo yake. Kutenda yaliyo sahihi na yenye faida sio tu kwake
mwenyewe bali pia kwa jamii yake na taifa lake.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA