Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga
marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita
kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katika mwaka ujao wa
masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia
kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.
Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma
certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa
kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo
yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya
kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.
Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma
shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu
kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi
daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za
kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa
diploma.
Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita
walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation
course haimuongezei mtu sifa.
"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za
kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa
kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa
fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course
haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza
Ndalichako.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA