Serikali
imesema kuwa ina mambo mengi ya kushughulikia katika elimu na siyo
mikopo ya elimu ya juu pekee, hivyo wanafunzi wanatakiwa kuwa
wavumilivu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi Mhandisi Stella Manyanya bungeni Dodoma, wakati akijibu swali la
nyongeza la mbunge wa Kilolo, Mh. Venance Mwamoto aliyetaka kujua hatma
ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaolalamika kukosa mikopo.
Mhandisi Manyanya amesema kuwa hadi sasa tayari awamu ya kwana ya fedha
za mikopo imekwisha toka, na kwamba kilichosababisha ucheleweshwaji ni
zoezi la uhakiki wa wanafunzi ili kupata wanafunzi wenye sifa sitahiki.
"Siyo kila muombaji wa mkopo atapata mkopo, mikopo hii itatolewa kwa
walengwa pekee ambao ndiyo wahitaji, serikali inashughulikia mambo mengi
katika sekta ya elimu na siyo mikopo pekee, kwahiyo pesa nyingine
zinatumika kwenye mambo mengine kama vile ujenzi wa mabweni, maabara na
miundombinu mingine"
Aidha Mhandisi Manyanya amewahakikishia wanafunzi kuwa tatizo la mikopo
litamalizika ndani ya wiki hii huku akisisitiza kuwa mikopo hiyo itakuwa
ni kwa walengwa pekee na siyo wanafunzi wote.
Kufuatia suala la mikopo hiyo kuanza kutikisa bunge katika kikao chake
cha kwanza hii leo, mwenyekiti wa kikao hicho ameiagiza serikali kuandaa
maelezo kuhusu sakata hilo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA