Tundu Lissu
Kwanza, nawasalimu makamanda wote na wapenda Maendeleo wote. Nawapa somo (Elimu Elimu Elimu).
Ile Benki yenye picha ya ndege imewatangazia wafanyakazi wake kuwa ipo
kwenye hali tete, wakae sawa kwa lolote litakalotokea hiyo ni kwa hapa
kwetu tu, ila nchini kwao iko vizuri na kwenye nchi nyingine iko vizuri
pia kutokana na mifumo mizuri ya huko.
Kumbuka kuna benki nyingine hivi karibuni, ile yenye jina la mnyama
mwenye shingo ndefu ilitangazwa kuwa ipo kwenye hali tete, pamoja na
hilo kuna Benki nyingine iliyokuwa kila mara inajitangaza kupata faida
nayo imepata hasara mwaka huu tutegemee kupata wategemezi wengi sana
kwenye familia kuanzia mwaka 2017.
Turudi tena kwenye point moja upende usipende wewe au mimi au wa kijani
(rangi ya mboga mboga) mjue tunaenda kwenye hali mbaya sana ya kiuchumi,
tunaenda kusoma namba, na Mzee wetu hataki kusikia hiki watu
wanachokilalamikia, anaongeza sheria tu,
siri-kali hailipi madeni ya ndani ila inadai kodi tu, kama unadaiwa na Benki kwa kukopa hiyo ni shauri yako.
Na hivi karibuni mmemwona kada maarufu wa kijani (aliyekuwa anasisitiza
ujasiriamali) anaidai siri-kali ila hajalipwa, izingatiwe amekopa benki
na atafilisiwa muda si mrefu na ataisoma namba kwani mali zake zitapigwa
mnada.
Nimetolea mfano mmoja tu kuna wananchi wengi tu mfano wahandisi,
wafanyabiashara waliiuzia bidhaa siri-kali au kutengeneza miundo mbinu
ya siri-kali hawajalipwa ila wanadaiwa kodi tu na vitisho chungu mbovu
na makampuni yao wamekopa benki wanashindwa kurejesha mikopo hiyo,
Vilevile yanashindwa kulipa kodi.
Sasa swali ni hili je?...
1. Mkifirisi mali zao na hamtaki kulipa madeni wanayowadai mtapata wapi
kodi kama hizo kwa kiwango kile kile tena baada ya kufilisi?
2. Na je, wafanyakazi watakao achishwa kazi kwenye kampuni mtakazo
filisi mali zao watapata wapi kazi tena katika kipindi hiki kigumu.
3. Na pia, jiulize kwa watakao maliza vyuoni na wenyewe watapata wapi tena kazi wakati wenzao waliopo kwenye kazi wanapunguzwa.
4. Na ukianzisha ujasiriamali kabla hujaanza biashara kodi unatakiwa
ulipe kwanza, kwa makadirio watakayo kukadiria wao siri-kali.
a) Usilete ushabiki wa kijani jiulize wewe unayefanya kazi kama uko salama?
b) Pengine utasema tuvumilie mambo yatakuwa mazuri , tafakari ujue wengi
watakuwa omba omba na uharifu utaongezeka, na uharifu ukiongezeka watu
watapandwa na hasira, na wakipandwa na hasira watamgeukia nani?
c) Mfano wewe mmoja ukibahatisha kazi nzuri utawasaidia ndugu zako au zetu wangapi?
Usitumie hasira kujibu!
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA