Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la polisi
kitengo cha usalama barabarani kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo
vya sheria mara moja madereva wanaotengeneza magari barabarani kwa
kuweka vizuizi vya mawe au matawi ya miti na kuondoka na kuendelea na
safari huku wakiviacha vizuizi vikiendelea kuwapo barabarani
Akitoa agizo hilo kwenye kikao cha 38 cha Bodi ya barabara Mkoa wa
Singida, Waziri Nchemba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba
Magharibi, amebainisha kwamba agizo hilo linalenga kutengeneza nidhamu
ya matumizi ya barabara pamoja na kuepusha ajali zisizokuwa na ulazima
wowote.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA