Diwani wa Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma na muimbaji, Baba Levo amedai kuwa kutokuwa na fedha ndio sababu iliyomfanya kuonekana kupotea kwenye muziki kwakuwa amekaa muda mrefu mrefu bila ya kuachia wimbo wowote.
Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa muziki kwa sasa ni biashara na kama hauna fedha huwezi kutoboa ndio sababu iliyomfanya akae muda mrefu bila ya kuachia wimbo mpya.
“Sababu kubwa iliyofanya nimeadimika kwenye muziki ni hela, kwa sababu sasa hivi muziki ni hela kama ni msanii mdogo mdogo na hela huna hata kama una kipaji cha nini shughuli inakuwa nzito sana kama huna hela,” amesema.
“Kwahiyo inanilazimu nikusanye fedha kwa ajili ya kurelease kazi zangu. Nimekuwa nikirelease ngoma kali lakini zimekuwa haziendi popote kwa sababu hela hakuna, kwahiyo hata kama una kipaji lazima uwe na mtu mwenye hela anasupport kipaji chako ndio utatoboa. Kipaji hakiwezi kukubeba hali imekuwa ngumu na muziki umekuwa biashara na biashara yoyote ni hela,” amesema Baba Levo.
“Kuwa diwani sio kuwa na hela, ukiona diwani yoyote ana fedha ndefu mrefu mwizi huyo tena hatari kabisa. Kuwa diwani hakukufanyi wewe kuonekana kuwa tajiri, hakukufanyi kuwa na hela nyingi. Kuna pointi moja tu, mimi diwani ni mwananchi kama wananchi wengine. Hali ngumu ikiwepo unakuwa kwetu sisi wote sio kama diwani ndio ninakuwa na fedha,” ameongeza
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA