Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kizota Mjini Dodoma, Yasin Abdallah, miaka 13, amekutwa amejinyonga bafuni nyumbani kwao baada ya kuchukizwa na kufanya vibaya katika masomo yake
Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Ernest Kimoli amesema tukio hilo lililotokea Desemba 2 eneo la Kizota Relini Manispaa ya Dodoma baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Hassan Juma, miaka 53 kugundua kujinyonga kwa mwanaye saa 6.00 mchana
"Sababu ya kujinyonga ni kuchukizwa na matokeo mitihani yake,"alisema
Diwani wa Kizota, Jamary Ngalya, alisema mtoto huyo ambaye alizikwa juzi jioni, alianza kwa kuwaeleza wanafunzi wenzake Ijumaa kuwa atajinyonga
Alisema baada ya kutamka hayo, wenzake walimwambia wanakwenda kumweleza mwalimu, hata hivyo baada ya kuwasikia wenzake aliwaambia kuwa anatania hawezi kufanya hivyo
Mwalimu mkuu wa Shule ya Kizota, Juma Malecela Mwanafunzi huyo alihamia Oktoba kutoka mkoani Kigoma
"Katika matokeo ya kumaliza darasa la nne alikuwa wa 129 kati ya 132 inawezekana huko alikuwa anafanya vizuri." alisema.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA