Msuva ‘on Fire’ Yanga Kileleni

Yanga imepaa hadi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya JKT Ruvu  katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili.


Ushindi dhidi ya JKT Ruvu unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 pointi moja mbele ya mahasimu wao Simba ambao watacheza kesho dhidi ya Ndanda FC mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili ya VPL.

Deusi Kaseke alifunga goli la kwanza la Yanga dakika ya 37 kipindi cha kwanza kwa kuunganisha pasi ya Simon Msuva

Msuva akafunga bao la pili dakika ya 57 kabla ya kufunga tena dakika ya 90 na kuilaza JKT Ruvu huku Yanga ikikaa kileleni mwa ligi ikisubiri matokeo ya Simba.

Lwandamina amepata ushindi wa kwanza katika mechi yake ya kwanza VPL baada ya kupoteza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya JKU ya Zanzibar.
Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ amepoteza mechi yake ya kwanza VPL tangu alivyoachana na Mgambo JKT ya Tanga na kuchukuliwa na TFF kuifundisha timu ya taifa ya vijana wa U-17 ‘Serengeti Boys.’
Ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa makocha wa timu zote ndani ya (Bakari Shime-JKT Ruvu na George Lwandamina-Yanga) Shime si mgeni wa VPL lakini amesimama kwa mara ya kwanza kama kocha wa JKT Ruvu wakati Lwandamina yeye ameisimamia Yanga kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa VPL.
Ushindi wa Yanga dhidi ya JKT Ruvu ni wa nane (8) mfululizo tangu mwaka 2013, timu hizo zimecheza michezo nane tangu mwaka 2013 na Yanga imeshinda mechi zake zote kwa zaidi ya magoli mawili.
17/12/2016 JKT Ruvu 0-3 Yanga

26/10/2016 Yanga 4-0 JKT Ruvu

07/02/2016 JKT Ruvu 0-4 Yanga

19/09/2015 Yanga 4-1 JKT Ruvu

25/03/2015 JKT Ruvu 1-3 Yanga

05/10/2014 Yanga 2-1 JKT Ruvu

06/04/ 2014 Yanga 5-1 JKT Ruvu

01/11/2013 JKT Ruvu 0-4 Yanga

Yanga imeshaifunga JKT Ruvu jumla ya magoli 29 katika mechi nane zilizopita huku yenyewe ikiruhusu magoli manne tu tangu mwaka 2013.

Chapisha Maoni

0 Maoni