MTATIRO: Ni kweli sijazungumza chochote kuhusu Ben Saanane, nasubiri 'findings' za taasisi yake

Anaandika Comred Julias Mtatiro
BEN!
Ni kweli kwamba sijazungumza lolote kuhusu comrade #Ben_Saanane, nasubiri FINDINGS za taasisi yake, CHADEMA, ili kupata mwelekeo. Tuendelee kuomba kokote aliko awe salama! Lakini kwa sasa yapo matarajio matano;
1. Ben kupatikana akiwa salama na akatueleza nini kilimkuta.
2. Ben kupatikana akiwa ameteswa, hajitambui na asiyejiweza tena siku za mbele.
3. Ben kupatikana akiwa mfu, marehemu au asiye na pumzi tena.
4. Ben kutopatikana kabisa, kupotea moja kwa moja, milele.
5. Ben kupotea kwa muda mrefu kisha kuonekana mbele ya safari (atatueleza nini kilimsibu).
Ni Mungu peke yake ndiye anajua nini kimempata na nini hatma yake, mimi na wewe hatuwezi kujua, tuendelee tu kumtafuta kwa kadri tuwezavyo.
Let us continue to close the fingers for Ben.
#TunamtakaBenakiwahai
#BringBackBenAlive

Chapisha Maoni

0 Maoni