Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga raia wa Burundi Amis Joslyn Tambwe ameelezea kinachompa kiburi na kuamini kuwa watatetea ubingwa wa Ligi kuu ya Tanzania bara VPL.
Tambwe amesema anaamini hakuna timu itakayowazuia Yanga kuwa mabingwa huku akitaja moja kati ya sababu zinazompa jeuri ni kucheza mechi nyingi wakiwa Nyumbani Dar Es Salaam.
Tambwe amesema Kucheza Ugenini kuliwafanya kuchoka sana ila Round Hii ya Pili mambo yatakuwa mazuri.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA