Wachezaji wa Yanga kwa umoja wao wameamua kumkataa Mchezaji mwenzao na ambaye pia ni Nahodha wa Klabu hiyo Nadir Haroub ‘ Cannavaro ‘ kwa madai kuwa amezidi na kukithiri kwa Umbea na kuwagawa Wachezaji.
Wachezaji hao wameenda mbali zaidi na kusema kuwa Mchezaji huyo Nadir Haroub ‘ Cannavaro ‘ amekuwa ni mpika majungu, mbea, mnafiki na mpelelezi wa Uongozi wa Yanga kitu ambacho amekuwa kila mara akipeleka maneno kwa Uongozi dhidi ya Wachezaji wa Yanga.
Wakizungumza na Mimi GENTAMYCINE asubuhi hii hii hapa maeneo ya Leaders Club ambapo sisi Wachezaji wa zamani huwa tunacheza Kiveterani zaidi kila Jumamosi na Jumapili na hawa Wachezaji huja kupata mawaidha yetu Wachezaji wapatao watano ( 5 ) ila kwa kutowaharibia huko Klabuni kwao sitowataja majina yao walikuwa wakizungumza na Mimi huku wakiwa wamefura ( kukasirika ) kabisa juu ya Vitendo vya Kinafiki vya Nahodha wao Cannavaro.
Wamesema kuwa tayari wameshakubaliana na wenzao wote kuwa kuanzia sasa hawamtaki huyo Mchezaji na kwamba hawatampa ushirikiano wowote ule na kuutaka Uongozi wa Yanga kama wameamua kuwawekea Mpelelezi basi ni vyema huyu Cannavaro awe anawekwa pale Magetini Uwanja wa Uhuru ili awe Mpelelezi kwa Viongozi wa Yanga ambao huwa wanapiga Hela za Viingilio na kwamba wakiendelea kumwacha awe nao kile walichomfanyia jana pale Uwanja wa Uhuru baada ya kumalizika kwa ile mechi dhidi ya African Lyon basi watamfanyia kitu mbaya zaidi na kwamba wamemchoka.
Ikumbukwe kuwa hii tabia ya Vilabu hivi viwili vya Simba na Yanga kumchagua Mchezaji mmoja kuwa Mpelelezi kwa wenzake haijaanza tu leo kwani huko nyuma Mchezaji na Kipa wa Simba Kelvin Mhagama nae alishawahi kupigwa mno na Wachezaji wa Simba akina Madaraka Selemani na Fikiri Magosso kwa tabia kama hizi anazofanya leo Nadir Haroub ‘ Cannavaro ‘ na kama haitoshi japo inafichwa fichwa hata Meneja wa sasa wa Simba Sports Club Mussa Hassan ‘ Mgosi ‘ hapendwi na Wachezaji wa Simba kwakuwa na yeye ni Mpelelezi wa Uongozi wa Simba kwani hata alipokuwa Mchezaji mwandamizi wa Simba alikuwa na tabia ya kuwapeleleza wenzake na kuwachoma kwa Uongozi na moja ya sababu kubwa ya kupewa Umeneja wa Klabu ya Simba ni baada ya kuwa mbea aliyetukuka kwa Vitendo vya Wachezaji wenzake.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA