Waziri Angela Kairuki atofautiana kauli na Katibu Mkuu Utumishi Dr. Ndumbaro

Serikali yawakana walioajiriwa mei mosi nukuu kutoka gazeti la Mwananchi, Dr. Ndumbaro akihojiwa na gazeti la Mwananchi amesema mikataba waliopewa ni batili.


Gazeti hilo hilo na,muandishi yule yule akamhoji Angela Kairuki
nanukuu "waziri wa ofisi ya rais ,menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ANGELA KAIRUKI Aalifanua ''hakuna mtumishi mpya wa umma ambaye ameingizwa kwenye payrol,KAMA WALIPANGIWA VITUO NA HAWAJAINGIZWA KWENYE PAYRoll wasubiri maelekezo "alisema Kairuki

Sasa Dr. Ndumbaro anasema walipewa mikataba batili,Angela Kairuki anasema kama walipangiwa vituo na hawajaingizwa kwenye payroll wasubiri maelekezo.

Ukweli ni huu
Hawa vijana wote walipangiwa vituo vya kazi,walipewa pesa za nauli na kujikimu,waliripoti kwenye vituo vya kazi,walipewa vitambulisho lakini hawakuingizwa kwenye payroll. Je, ubatili wao upo wapi?

Chapisha Maoni

0 Maoni