Chelsea wazidi kuuteka ulimwengu wa soka ligi kuu Uingereza

Chelsea
Mechi 6 za EPL, Ligi Kuu England, za kufunga Mwaka 2016 zimechezwa hii Leo na mechi moja inachezwa Usiku huu na Matokeo hadi tunapoweka habari hii Manchester City wako Nyuma kwa goli moja Dhidi ya Liverpool.
Zifuatazo ni Taarifa za Mechi za Vinara Chelsea walipocheza na Stoke City huko Stamford Bridge na nyingine huko Old Trafford kati ya Manchester United na Middlesbrough ambao ni maarufu kama Boro.

CHELSEA 4 STOKE CITY 2
Vinara wa Ligi Chelsea wamekwenda Pointi 9 mbele baada ya kuichapa Stoke City 4-2 na kuifikia Rekodi ya Arsenal ya kushinda Mechi 13 mfululizo za Ligi hii waliyoiweka Msimu wa 2001/02.

Bao za Chelsea hii Leo zilifungwa na Cahill, Dakika ya 34, Willian, 57 na 65, na la Diego Costa la Dakika ya 85.

Bao za Stoke zilipigwa Dakika za 46 na 64 kupitia Martins Indi na Peter Crouch. 

MANCHESTER UNITED 2 MIDDLESBROUGH 1
LICHA ya maamuzi mabovu ya Refa Lee Mason ikiwemo kuwanyima Bao safi la Zlatan Ibrahimovic, Manchester United walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kusawazisha Dakika ya 85 na Dakika moja baadae kupiga Bao la ushindi katika Mechi waliyoitawala kabisa.
Manchester United

Kipindi cha Kwanza, Man United walifunga Bao safi kupitia Ibrahimovic na Refa Mason kulikataa na Gemu kubakia 0-0 hadi Mapumziko.

Kipindi cha Pili, Dakika ya 67, bila kutegemewa, Boro walitangulia kufunga kwa Bao la Grant Leadbitter na kuelekea kumpa Msaidizi wa zamani wa Jose Mourinho, Aitor Karanka, ambae ni Meneja wa Middlesbrough, ushindi huku Kipa wa zamani wa Man United Victor Valdes akiwa nguzo yao imara akiwanyima Man United bao kadhaa za wazi.
Manchester United

Lakini Dakika ya 85, kazi njema ya Ibrahimovic ilimpa mwanya Anthony Martial kusawazisha na Dakika 1 baadae Krosi ya Juan Mata, alieingizwa Kipindi cha Pili, kuunganishwa kwa Kichwa na Paul Pogba na kuwapa ushindi Man United wa 2-1 wakikumbusha enzi za Sir Alex Ferguson za ushindi murua wa Dakika za mwisho hasa Leo ikiwa ni Siku ya Kuzaliwa ya Lejendari alietimiza Miaka 75 akiwepo pia Uwanjani hapo Old Trafford kushuhudia Mechi hii.

MOURINHO AKIONGELEA KWANINI BAO LA IBRAHIMOVIC LIMEKATALIWA:
“Refa Bwana Mason ndie anaejua lakini anajua alifanya kosa. Nadhani inasikitisha kwa sababu Marefa wanasikitika wakifanya makosa!”



VIKOSI: Manchester United (4-3-3): De Gea, Valencia, Bailly, Smalling (Rashford 72), Blind (Rojo 64), Herrera, Fellaini (Mata 64), Pogba, Mkhitaryan, Ibrahimovic, Martial.
Subs not used: Romero, Jones, Lingard, Schweinsteiger
Goals: Martial 85, Pogba 86
Booked: Blind

Middlesbrough (4-5-1): Valdes, Chambers, Bernardo, Gibson, Friend, Traore(Fabio 82), Leadbitter(Clayton 78), Forshaw, De Roon, Downing(Ramirez 64) Negredo.

Chapisha Maoni

0 Maoni