Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza kuwa kuna maduka mengi ya kubadili fedha (Bureau de Change) ambayo yanatumika kutakatisha fedha za dawa za kulevya, wasimamizi wa maduka hayo wameeleza kutoshiriki, bali wanafuata utaratibu uliowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa nyakati tofauti wamesema kabla ya kuuza au kununua fedha za ndani na nje ya nchi, hupewa utaratibu ambao ni lazima waufuate.
Akizungumza juzi wakati wa kukabidhi majina 97 ya watuhumiwa wa uuzaji wa dawa za kulevya, Makonda amesema jijini Dar es Salaam kuna maduka ya kubadilishia fedha takriban 220 na nchi nzima yapo zaidi ya 400, hivyo utitiri wa maduka hayo unarahisisha kuingiza fedha za dawa za kulevya kwenye mzunguko na kusaidia kutakatisha fedha haramu.
Meneja wa duka la kubadilishia fedha la TK, Tukuza Amri amesema ndiyo kwanza amesikia tuhuma hizo kwa sababu wao hufuata kanuni na utaratibu wa BoT.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA