HABARI PICHA: Mtama waifurahia kampeni ya ya TGGA ya hedhi kwa wasichana

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akitoa elimu kwa wanafunzi kuhusu Hedhi salama kwa wasichana  (Manustretion Hygiene) wakati wa kampeni iliyoendeshwa na chama hicho  katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi. 
Na Richard Mwaikenda, Mtama
WALIMU na Wanafunzi Mkoa wa Lindi, wamefurahishwa na Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyofanyika kwa uwazi katika Shule ya Sekondari Mtama.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa juzi na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mjini Lindi, yalishirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari pamoja na walimu katika Jimbo la Mtama.

Akielezea kuhusu kampeni hiyo, Mwanafunzi Fasda Mahamudu wa Shule ya Sekondari Mtama, alisema kuwa mafunzo aliyoyapata yamemfanya aelewe vizuri kuhesabu siku zake za hevi na jinsi ya kuwa msafi ikiwemo kuoga mara tatu kwa siku na kila baada ya kupata haja.

Naye Amana Amah mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Likongopele, alisema amefurahishwa na kampeni hiyo iliyoendeshwa kwa njia ya uwazi na kwamba imemfumbua mambo mengi ikiwemo kuzijua aina mbalimbali za pad za kisasa na jinsi ya kuzivaa wakati wa hedhi. Aliomba TGGA kuieneza kwa uwazi elimu hiyo katika shule mbalimbali vijijini.
Naye Mratibu Elimu Kata ya Mtama, Marcelinus Lukanga, aliwataka wasichana kujiunga kwa wingi TGGA ili waondokane na woga, hofu na kutokuwa na aibu jambo ambalo pia litawasaidia kuwa huru, safi, salama na kutopata kirahisi maambukizi hasa wakati wa hedhi.

Pia aliwashauri akina baba na kaka kutokuwa mbali na wasichana kwani nao ni wajibu wao kuwasaidia na ikiwezekana kuwapatia msaada wa hali na mali ikiwemo kuwanunulia vifaa vinavyowafaa wakiwa hedhi.

Mwalimu Mariamu Hashima wa Shule ya Msingi Lihimba, aliiisifia kampeni hiyo kwa kuendeshwa kwa uwazi na ukweli, lakini alishauri kuwa mafunzo hayo yatenganishwe kwa watoto wa shule za msingi kuwafundisha zaidi jinsi ya kujiandaa kupata hedhi na vifaa anavyopaswa kuwa navyo.

Timu ya kampeni hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba, Mkufunzi Msaidizi Rehema Kijazi, Kiongozi wa Girl Guides Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth, Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango.
 Wanafunzi wakishangilia baada ya kufurahishwa na elimu ya hedhi salama
 Mmoja wa viongozi wa Girl Guides Happiness akihamasisha wakati wa kampeni hiyo
 Walimu kutoka shule mbalimbali Jimbo la Mtama, wakisikiliza kwa makini wakati wa kampeni hiyo
 Rachel ambaye ni Girl Guides kutoka Uganda, akiwalekeza wasichana jinsi ya kutengeneza pad
 Girl Guides kutoka Madagascar akionesha namna ya kutengeneza pad
 Michelle Girl Guides kutoka Rwanda ambaye yupo nchi katika exchange program akionesha jinsi ya kutengeneza pad ya kawaida
 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akihutubia na kuwahamasisha wanafunzi wasichana kujiunga na TGGA
 Mratibu Elimu  Kata ya Majengo, Marsenus Lukanga (kulia) akimkabidhi kasha la vihifadhi (Pad),  Mwanafunzi wakati wa Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama (Manustretion Hygiene) kwa Wasichana iliyoendeshwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi.
 Viongozi wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi waliokabidhiwa makasha ya vihifadhi ya pad zitakazogawiwa kwa watakaopata hedhi shuleni kwao.
 Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed akimkabidhi zawadi ya pad Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtama, Asha Namjupa.
Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed akimkabidhi zawadi ya pad Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtama, Asha Namjupa.

Chapisha Maoni

0 Maoni