Msimamo wa baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi juu ya kuizuia Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifungo na Uvuvi ya mwaka 2017-2018 hadi pale watakapopata majibu yenye kueleweka juu ya hatua ya rasilimali ya mchanga kuhodhiwa na Serikali badala ya wananchi wenyewe kama ilivyokuwa awali utapata majibu leo wakati waziri wake, Hamad Rashid atakapojibu hoja zao.
Hatua ya wajumbe hao imetokana na malalamiko ya wananchi waliokuwa wakimiliki mashamba ambayo sasa yanachimbwa mchanga chini ya uangalizi wa Serikali huku wao wakiambulia patupu.
Awali, mashamba hayo yalikuwa yapo chini ya wananachi ambao walikuwa wakiyatumia kuvuna na kuuza mchanga huo kwa wamiliki wa magari na kampuni mbalimbali za ujenzi.
Mwakilishi wa Mfenesini, Machano Othman Said alisema pamoja na rasilimali hiyo kuonekana kupungua kwa kiwango kikubwa, haikusatahili wananchi kupokonywa mashamba yao bila makubaliano maalumu.
Mwakilishi wa Kijitoupele, Ali Suleima Ali ‘Shihata’ alisema utaratibu uliowekwa na Serikali juu ya mchanga ni hatari na unahitaji kufanyiwa marejeo ili kuepusha athari zinazoweza kuepukika.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA