Baada ya Simba kufanikiwa kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, imeelezwa kuwa gharama za kusajili wachezaji nyota zimeongezeka.
Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la shirtikisho, wataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, wakati mabingwa wa Ligi Kuu Young Africans watapeperusha bendera ya nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katibu Mkuu wa Young Africans, Boniface Mkwasa, alisema msimu huu watalazimika kuongeza bajeti kwa sababu wachezaji wamekuwa na nafasi zaidi ya moja katika kufanya uamuzi wa timu za kujiunga nazo.
Mkwasa alisema wakati Simba ilipokua haiwakilishi nchi kimataifa, gharama za usajili wa wachezaji zilikuwa za kawaida, lakini msimu huu mambo yamebadilika.
“Kiukweli uhitaji sasa umeongezeka, uhitaji umekuwa mkubwa, kila upande unahitaji kujiimarisha, kiasi cha fedha wanachotaka kimeongezeka na hii inatokana na kuwa na uhakika wa kucheza mashindano ya kimataifa,” Alisema Mkwasa.
Alisema misimu miwili iliyopita klabu yake ilikuwa na uwezo wa kusajili kabla ya ligi haijamalizika, lakini msimu huu hilo halijawezekana.
Baadhi ya wachezaji wa Young Africans ambao wamegoma kusaini mikataba mipya na sasa wako huru ni pamoja na Ngoma, Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Ally Mustapha ‘Barthezn na Simon Msuva.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA