Ukweli Mchungu..Askari wa Bunge, Wabunge wa CCM Mjipiime Upya. Hawa Wabunge wa Upinzani Tumewaagiza Sisi Walipa Kodi


Nina maswali yananitatiza sana kichwani kwangu juu ya nani mwenye mamlaka ya kulitumikia taifa bila bughuza na kuheshimiwa mawazo yake.

Jana nilikuwa natizama bunge, nikastaajabisha kuona wabunge wa CCM kuanza kumshambulia kwa maneno mbunge wa CHADEMA Mh. John Mnyika huku wakikataa kufuta kauli zao huku wakiwa comfortable bila wasiwasi wowote.

Naona jinsi gani mbunge yule kijana mdogo kabisa anavyovunjwa moyo na wabunge wenye uwezo mdogo ambao hawakuweza kulinyasua kivyovyote taifa hili maskini kwa miaka kibao japo wapo katika chama tawala, mfano yule mbunge wa mtela ambako hali yake siyo nzuri kabisa unaweza sema ni kati ya majimbo duni kabisa hapa Tz.

Swala la pili:- Najiuliza kwanini viongozi wa bunge na wabunge wanataka bunge liwe lilelile la kukubali kila kitu na hawataki akili mpya na mawazo mapya yatolewe ili kujitathmini na kuliendeleza taifa na siyo kila siku hali kuwa ileile ya kukubali kila kitu? Nani amewaambia kwamba sisi watanzania tunavutiwa zaidi na wanachotaka wao na sio mawazo yenye kuhoji kama akina Mnyika?

Kwann viongozi wa bunge wanataka wabunge wa upinzani wawe kama watoto wakiwa ambao hawana uhalali na nchi hii na wabunge wa CCM wawe comfortable kama kwamba nchi ni yao peke yao?

Mwisho, hivi hawa walinzi wa bunge kwanini hawana staha kwa viongozi wa upinzani kusema kwamba wao wameajiliwa na CCM na hao wanaowasukuma sukuma kwa dharau siyo viongozi wao na hawatakuja kuwa viongozi wa juu kabisa wa nchi hii, askari wa bunge wajia asses upya, hawako fair hata kidogo, wanalipwa na kodi za hao wanaowasukuma kama Mbwa na siyo vingine.

Chanzo JF

Chapisha Maoni

0 Maoni